Saturday, September 10, 2011

Abiria 250 waokolewa katika ajali ya meli ya Mv Spice Islanders


Hii ndiyo meli ya My Space Islader ikionekana ubavuni mara baada kupinduka na kuzama katika Bahari ya Hindi huko Nungwi Zanzibar usiku wa kuamkia leo , meli hiyo ilikuwa na abiria 610.

Watu 250 wameokolewa wakiwa hai katika meli iliyozama ya Mv Spice Islanders iliyokuwa ikitokea Bandari ya Malindi Unguja kuelekea Bandari ya Wete Kisiwani Pemba.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,Mohamed Aboud Mohamed amesema watu hao wameokolewa na Vikosi vya uokoaji na wananchi mbalimbali wanaotoa msaada wa uokozi katika tukio la kuzama kwa meli hiyo huko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Waziri Aboud amesema watu hao wamesafirishwa kwa kutumia Boti zinazokwenda kwa kasi za Zanzibar ambazo ilikwenda kutoa msaada katika eneo la tukio.

Amesema watu hao baada ya kufika Bandari ya Malindi Unguja watapelekwa Viwanja vya Maisara kwa ajili ya kuungana na familia na jamaa zao.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein yupo katika eneo la tukio huko Nungwi ili kujionea hali halisi ya tukio hilo

Source: Fullshangwe.blogspot.com

1 comment:

  1. BIG MOUTH ONLY,TOMUCH KNOW, NO ONE KNOWS ANYTHINGS,THERE IS HYPOCRITE AND HELL WILL BE THEIR HOME

    ReplyDelete