Friday, September 23, 2011

Je, tunakwenda wapi?

ASI ZAIDI!! NGUVU ZAIDI!! NA HARI ZAIDI!! TULIAHIDI NA TUMETEKELEZA!! NA NYINGINE; TUMEWEZA! TUMETHUBUTU! TUNASONGA MBEEELEEE!! YA MWISHO NAYO; PIPOOO!!! PAWAAAA!!!


Hii ni moja ya Shule ya msingi Bukoba – Kagera

'HIZO ZOTE NDIO KAULI ZA WANASIASA'
Wanasiasa watatujia kwa kauli nyingi sana, lakini mwisho wa siku watoto wetu tunaishia kuwapa elimu kwenye mazingira kama haya! ebu muangalie huyo aliye karibu na Mfuko wa plastic, yupo darasani kweli!!! nini anachowaza! Mimi na wewe tutabaki tunahisi tu: Labda hajanywa chai! au anaumwa! La hasha! mazingira hayo yanampelekea kutomsikiliza mwalimu.


Wanafunzi wa Shule ya Msingi huko Ludewa Mkoa mpya wa Njombe wanasoma kwenye Kanisa, Wizara husika zinayajua haya kweli ya watoto wetu ambao ni Taifa la Leo na kesho!

Chanzo: KAPINGAZ Blog

No comments:

Post a Comment