Wednesday, September 14, 2011

Mwalimu afanya mapenzi na mwanafunzi darasani


Mwalimu was shule yamusingi yaOthandweni, Swaziland anatuhumiwa kumbaka mwanafunzi wa miaka 15 darasani wakiwemo wanafunzi wenzake. Tukio hili la ajabu lilifanyika wakati wa somo ya hisabati mbele ya wanafunzi wengine.

Gazeti la Swazi Observer limeripoti kwamba tendo hili la ajabu lilifanyika wiki mbili kabla shule kufungwa kwa ajili ya mapumuziko ya mhula wa pili wa masomo. Shule zilifungwa wiki mbili zilizopita.

Mwalimu huyu sasa hivi anachunguzwa na polisi.

Anatuhumiwa kufanya mapenzi na mwanafunzi ambaye kisheria hakuwa na ridhaa ya kufanya hivyo kutokana na umri wake mdogo.

Mwalimu huyo anatuhumiwa kwamba aliwaambia wanafunzi wengine waendelee na masomo au wafumbe macho na wasijali kitendo kilichokuwa kinaendelea mbele yao.

Vyanzo vya habari vilisema aliendelea kukunjua sare ya msichana huyo na kufanya mapenzi naye.

Baada ya kuwaamuru wanafunzi wafumbe macho na waangalie upande wa ukuta, kelele zilizokuwa zinapigwa na mwalimu huyo zilisababisha wafumbue macho.

Walipogeuka, walishangaa, kuona mwenzao sare yake ikiwa imekunjwa akiwa amemkumbatia mwalimu wake.

“Sikuamini tendo lilikuwa likitokea. Tulipomsikia akipiga kelele, tulifumbua macho,” mmoja wa wanafunzi hao alisema.

Mkuu wa shule hiyo alisema kwamba yeye ameliona tukio hilo kuwa ni la ajabu hivyo aliwaachia polisi waendelee na uchunguzi.

No comments:

Post a Comment