Monday, September 26, 2011

Taswira ya jamii


Mbwa wa polisi akiwa uwanjani peke yake baada ya kuwafukuza wachezaji.


Ndani ya Uwanja wa CCM kirumba mwanza lilitokea tukio la aina yake baada ya Mbwa wa Polisi kuingia uwanjani na kuanza kukimbiza wachezaji wakati wa mechi ya Simba na Toto Africa.

Kitendo kama hiki cha kizembe ni nani alaumiwe! na TFF imesemaje ili kisitokee tena?
Kwa uelewa wangu Mbwa wa polisi akipelekwa kwenye shughuli za Soka anatumika tu kwa ajili ya kutishia wale ambao wanataka kukiuka taratibu, lakini sio kwa kumuachia kama hivi. Kama hii mechi ingekuwa ni ya Kimataifa TFF wategemee nini kutoka FIFA! au Fideration ambayo itakua imeandaa mashindano hayo!


Madereva wa Mabasi na Matrafiki katika Stand kuu - Mbeya.

Tukio la Madereva wa Mabasi ya masafa marefu kutoka Mbeya kugoma kuendesha mabasi yao kwa kulalamikia 'TOCHI' nyingi barabarani limenishangaza sana, kwa faida ya wasioelewa, TOCHI ni Kamera za usalama barabarani zinazotumiwa na Matrafiki kuangalia magari yanayokwenda mwendo wa kasi katika eneo ambalo hawastahili kwenda mwendo huo.

KAPINGAZ Blog

No comments:

Post a Comment