Thursday, February 9, 2012

Mtahiniwa aliandika verse kwenye karatisa yake ya majibu ya mtihani

Baraza la mitihan la Taifa (NECTA)limewafutia matokeo yao watahiniwa
elfu 3,303 baada ya kugundulika kufanya udanganyifu na kutumia
lugha chafu kwenye mitihani yao ya kidato cha nne iliyofanyika oktoba 2011 ambapo katika hali isiyo ya kawaida mmoja wa watahiniwa hao aliamua kuandika katika karatasi yake wimbo wa bongo fleva.

Katibu mtendaji mkuu wa baraza hilo Dr Joyce Ndalichako amesema “nashukuru sana wote wanaosahihisha huu mtihani wangu, nitakapofeli nitaendelea na fani yangu ya bongo fleva, majita yangu yako levo za juu na sio East zuu, ukiona vyaelea ujue vimeundwa”

Joyce amesema mtahiniwa aliandika mistari katika kila sehemu alipotakiwa kujibu swali, swali la sita na la saba aliandika hiyo mistari hapo juu, swali la kumi na moja ameandika “acha utani my girl, unauja nyumbani umezizi, mwenzako huku naona sijiwezi, kazi hiyo ya kuzizi nakwambia ukweli mwanzo ulikua mzuri lakini mwisho ukawa mbaya”

kwenye sentensi nyingine Katibu huyo mkuu amesema “katika mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana watahiniwa laki mbili na elfu 25 sawa na asilimia 53.37 wamefaulu huku kati yao wasichana ni elfu 90 na 885 sawa na asilimia 48.25 na wavulana ni laki moja na elfu 34 sawa na asilimia 57.51.

Shule ya sekondari ya wasichana ya St. Francis Mbeya imeongoza kwa shule kumi zilizofanya vizuri, ambapo katika wanafunzi waliofaulu vizuri sana wameongozwa na Moses Andrew Swai kutoka shule ya sekondari ya Feza iliyopo jijini Dar es salaam.

Source: Bonyeza24 blog

No comments:

Post a Comment