Wednesday, August 3, 2011

Zombe 'atishia' kujinyonga


Aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Abdalah Zombe akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam jana asubuhi.

Katika maelezo yake Zombe alisema kuwa anamshangaa Mbunge wa Arusha mjini, ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ,Godbless Lema kwa kitendo chake cha kuhoji kuhusu uhalali wa hukumu ya Zombe katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya Mauaji ya wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge.

Zombe alisema kuwa Lema, haijui Katiba ya Tanzania na kufafanua kuwa Lema kama mbunge, Bunge ni muhimili wa Dola unaojitegemea na vile vile pia Mahakama ni muhimili wa Dola unaojitegemea. Hivyo alimshangaa Lema kuwa hakutakiwa kuhoji maamuzi halali ya Mahakama.

Aidha aliongeza kusema kuwa Wabunge wa CHADEMA hawajui watendalo bungeni na kuwa endapo Chadema watapata ridhaa ya kuongoza nchi, yeye Zombe atajinyonga.

"Endapo kama CHADEMA watatawala nchi hii, mimi nitajinyonga kabisa" Hiki ni chama cha hovyo na wabunge wake ni wa hovyo. "Hawaijui Katiba",alisema.

Zombe alimaliza kwa kusema kuwa anamfahamu Lema siku nyingi na kwamza alikuwa ni mmoja kati ya wanamtandao wa wizi wa magari kutoka nchini Kenya akiwa na wenzake.

Source: Daily Mitikasi

No comments:

Post a Comment