Monday, September 12, 2011

Bomba la Mafuta lalipuka Kenya, la uwa mia

Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa takriban watu 100 wameuawa na moto baada ya bomba la mafuta kulipuka katika eneo la viwanda Lunga Lunga jijini Nairobi, Kenya. Wazima moto wanajaribu kuzima moto huo.

Tulkio hilo lilifanyika baada ya siku mbili watu takribani mia mbili wamepoteza maisha baada ya meli ya MV Spice Islander kupinduka na kuzama baharini ikitokea Unguja ikielekea Pemba.


Rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (SMZ) Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wawili wa Rais wa Zanzibar, Waheshimiwa Seif Sharif Hamad na Balozi Seif Idd, Rais Mstaafu wa Zanzibar Mheshimiwa Amani Abeid Karume na uongozi karibu wote wa juu wa SMZ wakitembelea Viwanja vya Maisara mjini Zanzibar kujionea wenyewe zoezi la kutambua miili iliyoopolewa kutoka baharini kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya MV Spice Islander alfajiri ya Jumamosi.

Pic: Full shangwe blogspot

No comments:

Post a Comment